Halmashauri ya Wilaya yaShinyanga ina vyanzo vingi vya maji kama vile visima na mito .Kiuhalisia upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Shinyanga bado haujaweza kuwafikia wananchi wote katika vijiji vilivyopo.
Huduma ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inatolewa kwa watu wapatao 218,246 ambao ni sawa na asilimia 60.04 ya wakazi wote Hivyo Idara inaendelea na jitihada zaidi za kutafuta rasilimali zitakazowezasha ujenzi wa miradi ya maji kutekelezwa hivyo kuboresha hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
Miradi hii inaweza tekelezwa kwa awamu kutegemea uwezo halisi na upatikanaji wa fedha. Kwa maelezo bonyeza hapa kupakua faili kupata maelezo ya kina.
Majukumu ya Idara ya Huduma za Maji
•Kutathimini, kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa sera za sekta ya maji katika ngazi ya wilaya.
•Kuendeleza na kuboresha hali ya huduma za maji na usafi wa mazingira katika wilaya.
•Kuwezesha, kuratibu, Kusimamia, na kuthibiti sekta binafsi zinazotoa huduma za Maji katika wilaya.
•Kuwezesha na kuratibu timu ya huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika wilaya.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.