Halmashauri katika Mkutano wake wa mwaka itateua Wajumbe wa Kamati za Kudumu zifuatazo ambazo zitakuwa na idadi ya wajumbe ( ukimwondoa Mwenyekiti wa Halmashauri isipokuwa katika Kamati ya Fedha na Utawala) kama inavyoonyesha hapa chini au kama itakavyorekebishwa na Halmashauri mara kwa mara.Isipokuwa katika kuteua Wajumbe wa kamati ya Fedha ,Utawala na Mipango Mwenyekiti na Mkurugenzi watazingatia uwiano wa uwakilishi wa vyama katika Halmashauri.
Kamati | Idadi ya Wajumbe
|
Akidi
|
(a) Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira | 16 | 5 |
(2) Kila Mjumbe wa Halmashauri atakuwa Mjumbe wa angalau Kamati moja ya Kudumu .Kamati ya Fedha na Utawala itakuwa na Wajumbe wafuatao:-
(a)Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye atakuwa Mwenyekiti.
(b) Makamu Mwenyekiti
(c) Mbunge au Wabunge wa Majimbo wanaowakilisha Majimbo katika eneo la Halmashauri.
(d) Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri
(e) Wajumbe wengine wasiozidi wawili (2) watakaopendekezwa na Mwenyekiti na kupigiwa kura na Baraza la Halmashauri mmoja kati yao awe mwanaume
Majukumu ya Kamati hii ni kama :-
(a) Kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Halmashauri
(b) Kutunga Sheria Ndogo
(c) Kuweka na kutoza kodi
(d) Kutoza ada na ushuru
(e) Kuidhinisha mpango na bajeti ya Halmashauri
(f) Kuingia mikataba mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikataba ya kukopa
(g) Kupitisha mpango wa utoaji huduma.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.