Hayo yamezungumzwa leo Novemba 15, 2024 na muwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Richard Luhende ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Didia wakati wa Bonanza la Michezo mbalimbali katika viwanja vya Shule ya Msingi Didia.
Mhe. Luhende ameongeza kuwa kwa kata ya Didia wamejiandikisha kwa asilimia 78 hivyo ni matumaini Wananchi wote waliojiandikisha watajitokeza kwa wingi kupiga kura.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Monica Mnanka amewakumbusha Wananchi kuhudhuria Mikutano ya Kampeni kwa wagombea itakayo anza tarehe 20 had 26 novemba ili kujua sera zao.
Zoeze la upigaji kula linatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 ambapo nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti wa kitongoji, wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi mchanganyiko pamoja na Wajumbe Halmashauri ya Kijiji Wanawake na kwa mujibu wa Serikali itakuwa siku ya mapumziko.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.