Hayo yamezungumzwa na Mhe. Wakili Julius Mtatiro wakati wa mashindano ya baiskeli yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Tinde A kata ya Tinde.
Wakili Mtatiro amesema baada ya kupokelewa Jokofu la kuhifadhia miili ya marehemu tayari amewasiliana na Bohari ya Dawa (MSD) kupeleka mashine ya X-ray katika kituo Cha Afya Tinde ili iweze kuwasaidia Wananchi pindi wapatapo changamoto za mifupa waweze kusaidiwa hapo.
Aidha, ameongeza kuwa ameletwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kutatua kero hivyo kuwataka Wananchi wote wenye changamoto za mirathi, kunyimwa dhamana polisi na kuonewa kwa namna yoyote kuwa huru kuwasiliana nae kupitia namba yake 0739420421
Kwa upande wa wananchi, Maria Mwita Chacha pamoja na Lucia Elias Salaganda wamemshukuru mkuu wa wilaya kwa kuendelea kuwahudumia na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kuleta maendeleo katika Kata ya Tinde.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.