Idara hii ina lengo la kusaidia au kuwezesha utoaji huduma na uendelezaji wa Elimu ikijumuisha usimamizi wa elimu ya sekondari na inayotolewa katika njia isiyo rasmi; na mitihani ya shule za sekondari, Seksheni hii inaongozwa na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya, ambaye anawajibika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Majukumu ya Idara ya Huduma za Elimu
•Kuratibu uongozi wa shule za sekondari.
•Kuratibu ajira na usambazaji wa walimu wa shule za sekondari katika Wilaya.
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Elimu na mafunzo ya ufundi ndani ya Wilaya na kutoa Ushauri kadiri inavyohitajika.
•Kusimamia mitihani ya shule za sekondari katika Wilaya.
•Kuratibu ukusanyaji, tathimini, uunganishaji/uandaaji, kutafsiri na kutoa taarifa/takwimu za elimu na mafunzo ya ufundi katika Wilaya.
•Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa taarifa za ukaguzi.
•Kuratibu shughuli zinazohusiana na michezo katika Wilaya na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Wilayani.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.