Sekta ya kilimo ndiyo inayotegemewa kwa kiasi kikubwa na wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kwani zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa eneo hili wanategemea kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku.
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ina Eneo lenye ukubwa wa jumla ya kilomita za mraba 4,212, kati ya eneo hilo, linalofaa kwa kilimo ni kilomita za mraba 1713.7. Mkakati uliopo ni kuendelea kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji kadiri bajeti itakavyoruhusu kwa lengo la kuendeleza kilimo cha umwagiliaji. Mazao yanayolimwa: Mpunga, Choroko, Dengu, Vitunguu, Mtama, Mahindi, Pamba, uwele nk.
1. Kusimamia na kuratibu ukaguzi mazao ngazi ya Halmashauri
2. Kusimamia mtandao wa mawasiliano ngazi ya Halmashauri.
3. Kuandaa utabiri wa uzalishaji mazao ngazi ya Halmashauri
4. Kufuatilia upelekaji wa taaluma ya uzalishaji mazao ngazi ya Halmashauri.
5. Kuratibu na kufuatilia Programu zote za ugazi katika eneo husika
6. Kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali na mashirika ya umma
yanayojihusisha na uzalishaji, usindikaji na uuzaji wa mazao
7. Kuandaa mahitaji na upatikianaji wa pembejeo
8. Kusimamia udhibiti wa visumbufu vya mazao na mimea katika ngazi ya Halmashauri
9. Kusimamia/ kuendeleza taaluma ya uzalishaji wa mazao ngfazi ya Halmashauri
10. Kutafsiri sera kuhusu uendeshaji na uzalishaji mazao.
11. Kuandaa/ kuandika taarifa ya utekelezaji wa sekta ya kilimo
12. Kuandaa program za uendelezaji mazao.
13. Kuratibu huduma za umwagiliaji kwa wakulima
14. Kufanya tathimini ya Mazingira kabla na baada ya miradi ya umwagiliaji
15. Kuwaelimisha wakulma juu ya sheria za kilimo
16. Kutoa ushauri wa kitaalmi juu ya matumizi ya pembejeo
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.