Idara hii ina lengo la kusaidia au kuwezesha utoaji huduma na uendelezaji wa Elimu ikijumuisha usimamizi wa elimu ya awali, msingi, na elimu ya watu wazima na inayotolewa katika njia isiyo rasmi; na mitihani ya shule za msingi, Seksheni hii inaongozwa na Katibu Afisa Elimu wa Wilaya, ambaye anawajibika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Majukumu ya Idara ya Huduma za Elimu
•Kuratibu uongozi wa shule za awali, Msingi, na elimu ya watu wazima na Elimu rasmi
•Kuratibu ajira na usambazaji wa walimu wa shule za awali, na msingi katika Wilaya.
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Elimu na mafunzo ya ufundi ndani ya Wilaya na kutoa Ushauri kadiri inavyohitajika.
•Kusimamia mitihani ya shule za msingi katika Wilaya.
•Kuratibu ukusanyaji, tathimini, uunganishaji/uandaaji, kutafsiri na kutoa taarifa/takwimu za elimu na mafunzo ya ufundi katika Wilaya.
•Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa taarifa za ukaguzi.
•Kuratibu shughuli zinazohusiana na michezo katika Wilaya na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Wilayani.
TAARIFA YA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA IDARA YA ELIMU MSINGI, 2016/2017
Shughuli |
Malengo
|
Mpango wa utekelezaji |
Utekelezaji |
Maelezo/maoni |
Kuboresha mazingira ya kujifunzia
|
Kuongeza Idadi ya shule za msingi zenye madarasa ya Elimu ya Awali kuongezeka
|
Kuongeza madarasa ya Elimu ya Awali kutoka madarasa 66
|
Madarasa 3 ya awali yamejengwa katika shule za msingi Didia, Mhangu A.
|
Watoto wote wenye umri wa miaka 5 hadi 6 kuanza Elimu ya Awali katika mazingira mazuri
|
Kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa madarasa ya awali ili wasiingiliane na wale wa shule za msingi.
|
Kuongeza matundu ya vyoo kutoka matundu.
|
Matundu ya vyoo 21 yamejenga, S/Msingi Kilimawe (11) na Masekelo (matundu 10)
|
Ufinyu wa fedha za utekelezaji mpango huu unakwamisha ujenzi wa vyoo vinavyohitajika.
|
|
Utengenezaji wa madawati.
|
Kutengeneza madawati 24,614 ili kutosheleza mahitaji.
|
Madawati 14,053 yametengenezwa na kununuliwa.
|
Utengenezaji unaendelea kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati.
|
|
Kuwepo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia
|
Kununua na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule zote 129
|
Kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kufikia uwiano unaotakiwa na Wizara kwa 1:1 kwa wanafunzi wote kupitia ruzuku ya Capitation na Development
|
Kila shule imenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
|
Ununuzi wa vifaa vya kufundishia unaendelea kadri upatikanaji wa fedha toka Serikalini.
|
Michezo ya UMITASHUMTA
|
Kuimarisha afya za wanafunzi na kukuza vipaji vyao.
|
Kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA kuanzia ngazi ya Shule hadi Taifa
|
Wanafunzi wa shule za Msingi 129 kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA
|
Michezo ilifanyika mwisho ngazi ya Kitarafa baada ya Mh. Rais kusitisha ngazi nyingine
|
Kuendesha mitihani ya MOCK kwa darasa VII na Mitihani ya Taifa kwa darasa la IV na VII.
|
Kuboresha taaluma ya wanafunzi
|
Kuendesha mitihani ya Mock mkoa na wilaya kwa darasa la VII na mitihani ya Taifa ya darasa la IV&VII. 2016
|
Mitihani ya Mock Mkoa na Wilaya kwa darasa la VII na mitihani ya Taifa ya darasa la IV&VII. 2016 kufanyika kwa umakini mkubwa.
|
. Ufaulu kuongezeka toka 61% kwa mwaka 2015 hadi 67% mwaka 2016.
|
Kuendesha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za Elimu ya awali na msingi.
|
Kuwa na takwimu sahihi za Wilaya.
|
Kuendesha zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Elimu ya Awali na Msingi
|
Zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za wanafunzi, miundombinu na samani za Elimu ya Awali,Msingi na lilifanyika kwa wakati.
|
Takwimu zilikusanywa na kupata jumla ya wanafunzi Awali hadi std VII - 2016 wapatao 73,841.
|
Kufanya ufuatiliaji katika shule msingi
|
Kuangalia na kuhimiza utendaji kazi wa walimu.
|
Kufanya ufuatiliaji wa shule zote msingi 129
|
Kufuatilia utoaji wa taaluma na Baadhi ya shule zilizokuwa na mambo yote ya kiutawala ,ili kuinua taaluma .
|
Baadhi ya Shule zilizofanyiwa ufuatiliaji na zilizoonekana kutofanya vizuri kitaaluma zilipewa onyo na kuhimizwa kufanya kazi kwa bidii.
|
Shughuli za Mradi wa Equip Tz. |
Kuboresha elimu ya msingi
|
Mafunzo ya KKK module 1-13
|
Walimu Wakuu, SBIC, na Waratibu Elimu Kata na DITs walipata Ruzuku.
|
Mafunzo yametolewa kwa walengwa.
|
Mafunzo ya WWJ 2016 Awamu I na II
|
Walimu wasaidizi wa jamii kutoka kata 27 walipata mafunzo
|
Mafunzo yametolewa
|
||
Ruzuku kwa Waratibu Elimu Kata
|
Waratibu elimu kata wote walipata mafunzo
|
Waratibu Elimu Kata wamepata Ruzuku yao.
|
||
Mafunzo ya Uongozi na Utawala wa Shule
|
Walimu Wakuu Wasaidizi, Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata, TOTs walipata mafunzo
|
Viongozi wamejengewa uwezo wa masuala ya uongozi.
|
||
Early Grade Mathematics (EGM) Moduli 1 - 4
|
Walimu Wakuu, SBIC,na Waratibu Elimu Kata walipata mafunzo hayo
|
Walimu wamepata mbinu mpya za ufundishaji wa somo la Hisabati.
|
||
Mafunzo SIS – kuhusu Matumizi ya vishikwambi na mfumo wa takwimu za shule.
|
Walimu wakuu
Waratibu elimu kata walipata mafunzo |
Walimu wakuu wa Waratibu elimu kata wanaendelea kuingiza taarifa kwenye mfumo.
|
||
Mafunzo ya kuanzisha klabu za JUU za shule.
|
Waratibu Elimu kata, Afisa Maendeleo ya Jamii kata Walimu Wakuu, Mratibu wa UWW, Walimu walezi na mjumbe 1 wa kamati ya shule walipata mafunzo shule zimebuni miradi ya kuongeza kipato cha shule
|
Uhamasishaji unaendelea
|
||
Mafunzo ya kubuni na kuanzisha miradi (IGA)
|
Waratibu Elimu kata na walimu wakuu walipata mafunzo
|
Shule zimebuni miradi ya kuongeza kipato.
|
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.