Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameongoza zoezi la upandaji miti siku ya madhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara Leo Desemba 9, 2024 katika shule ya msingi Mhangu B iliyopo kata ya Salawe Kijiji Cha Songambele.
Wakili Mtatiro akiambatana na Viongozi wa Dini, Wakuu wa Idara pamoja na wananchi wamepanda miti 1000 ili kutengenze na kufanya mazingira ya shule yawe rafiki kwa wanafunzi.
Aidha Wakili Mtatiro amewasihi wananchi kuwa zoezi hili la upandaji miti liwe endelevu huku akiagiza Viongozi wa Serikali za Mitaa kupitia vikao vya Kijiji kusimamia zoezi hili la kila kaya kupanda miti ili kuendelea kuweka Dunia yetu ya kijani.
Awali akimaribisha mgeni rasmi Ndg. Robert Anastory Kaimu Mkuu Kitengo Cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amesema zoezi hili limelenga kutekeleza agizo la upandaji miti kwa ajiri kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.