Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ndicho chombo cha juu cha maamuzi yote ya Halmashauri.Baraza la Madiwani hufanya maamuzi ikiwa pamoja na kutunga sheria ndogo, kupitisha sera na miongozo mbalimbali.
Baraza la madiwani linaundwa na jumla ya madiwani 35.Vilevile,baraza la madiwani linakaa angalau mara moja kwa miezi mitatu (3).
Katika utaratibu wa kawaida Baraza la Madiwani hupokea na kujadili taarifa za maendeleo kutoka katika kamati za kudumu za Halmashauri ambazo ni kamati ya fedha na uongozi, kamati ya Elimu, Afya na Huduma za Uchumi pamoja na kamati ya Mipango Miji na Mazingira.Baraza la madiwani ndiyo mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa Halmashauri.
Aidha, baraza la madiwani limepewa mamlaka kisheria kuwapandisha vyeo na kuwashusha vyeo watumishi katika utendaji wao wa majukumu waliyopewa.
BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.