ZIARA YA MKUU WA WILAYA, KIJIJI CHA MUONGOZO KWA AJILI YA UTOAJI ELIMU YA UMILIKI WA ARDHI NA UTHAMINI KWAJILI YA FIDIA
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akiambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya , Wataalam kutoka Tume ya Madini, Mthamini wa Ardhi pamoja na Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Simon Berege. Amefanya mkutano na Wananchi pamoja na wamiliki wa Mashamba ambayo yapo katika Eneo la muwekezaji wa uchimbaji madini, Kwaajili ya kutoa Elimu ya umiliki na matumizi bora ya ardhi kisheria sambamba na uwekezaji katika sekta ya madini.
Mkutano huo umefanyika Ofisi ya Kata zilizopo Kijiji cha Muongozo, Kitongoji cha Nyandolwa kata ya Mwenge.
Mhe. Mkuu wa Wilaya akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Muongozo, Kata ya Mwenge amewataka kufwata taratibu na sheria zilizowekwa na kuhakikisha Elimu iliyotolewa na Wataalm inaleta manufaa na kuepusha migogoro baina ya Wananchi, Wamiliki wa Ardhi na Wawekezaji. Kutokana na uwepo wa Rasilimali asilia ( Madini) katika maeneo hayo.
Aidha, alisisitiza Jamii pamoja na Uongozi kushirikiana na Wawekezaji kwa kufwata Sheria, Taratibu na Kanuni katika kutekeleza majukumu ya kuiendeleza Jamii ya Muongozo na kudumisha Amani.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.