Kikao hicho kimefanyika Disemba 4, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi za Mkuu wa Mkoa Shinyanga. Kikao hicho kilihudhuliwa na baadhi ya Maafisa na Watumishishi wa Wizara ya Ardhi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga, Wenyekiti wa Halmashauri na Wabunge kutoka Majimbo ya Mkoa wa Shinyanga.
Waziri silaa amefika Mkoani Shinyanga kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya Ardhi.
Mhe. Jerry Silaa amewataka Watumishi wa Sekta ya Ardhi kubadilika na kufanya Kazi kwa weledi na kuwatumikia Wananchi kwa kuzoingatia taaluma zao.
Kwa upande wake Kamishina wa Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Shinyanga Leo Komba amesema Mkoa wa Shinyinga umefanya Kazi maelekezo yote ya Baraza la wizara huku akiahidi kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri za Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akitoa salamu za Halmashauri alisema kumekuwa na migogoro sugu ya Ardhi kati ya Halmashauli ya Nyag’wale na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kupitia Kijiji cha Chang,ombe. Mhe. Silaa alimuelekeza Katibu Mkuu na Msajili wa Mabaraza kufika Shinyanga.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.