Maafisa Maendeleo kutoka Makao Makuu ya Wilaya pamoja na mdau kutoka shirika la PAWWCO wawatembelea wazee wenye matatizo ya ukoma katika kata ya usanda kjiji cha ngaganulwa.Wazee hao wanalelewa chini ya uangalizi wa kanisa katoliki lililopo usanda ,jumla ya wazee wanaolelewa katika kituo hicho wapo 14 ,wakiwemo wanaume watano (5) na wanawake tisa (9).
Wazee hao walipatiwa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni,nguo pamoja chumvi.
Afisa Maendeleo Wilaya Bw.Deus M.Muhoja akikabidhi miche ya sabuni kwa Bi.Maria kutoka katika kituo cha kulelea wazee wenye matatizo ya ukoma.
Afisa Maendeleo kutoka Makao Makuu ya Wilaya Bi.Aisha M.Omary akikabidhi miche ya sabuni kwa Bi.Elizabeth ambae ni mmojawapo wa wazee wanaolelewa katika kituo hicho.
Mdau kutoka shirika la PAWWCO akimkabidhi nguo makamu mwenyekiti wa wazee katika kituo hicho Bw.Zakaria Makaranga .
Makamu Mwenyekiti wa wazee Bw. Zakaria Makaranga akitoa neno la shukrani kwa msaada wa vitu mbalimbali walivyokabidhiwa.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.