Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya afya ya akili na jinsi ya kupambana na Msongo wa Mawazo yaliyoandaliwa na Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wakishirikia na kitengo cha Ustawi wa Jamii, leo 26 Septemba 2024 katika ukumbi wa Halmashauri.
Akitoa utangulizi kabla ya mafunzo Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndg David Rwazo amesema kufanya mafunzo haya ni maagizo ya serikali na hii ni kutokana na changamoto nyingi zinazotokana na Msongo wa mawazo kwa watumishi.
“Watu wengi wamekuwa wanafanya mambo hayo kwa kukosa upendo kiasi kwamba ndugu wenyewe kwa wenyewe Pamoja na watumishi ndani ya taasisi kumekuwa na mafarakano” Ndg Rwazo
Mafunzo hayo yameendeshwa na Dk Joeph Malima mratibu wa huduma za afya ya akili Mkoa wa Shinyanga ambaye amebainisha viashiria vya changamoto za afya ya akili kuwa ni mtu kujitenga, kuwa na mawazo mengi, shida katika kupata usingizi,kupoteza uwezo wa kumbukumbu, kula sana Pamoja na wasiwasi uliopitiliza.
Dk Malima ameongeza kuwa kuna madhara mengi unaweza kuyapata mtumishi kama utashidwa kupambana na changamoto hizo ikiwemo magonjwa ya moyo, maumivu ya mwili, Ngozi kufubaha na shida katika mfumo wa umeng’enyaji chakula.
Aidha ameshauri watumishi kushiriki katika mazoezi, kula chakula bora, kuchanganyika na wengine, kupata muda wa kupumzika ikiwa ni Pamoja na kukutana na na wataalamu wa tiba za afya ya akili na viongozi wa dini kama changamoto ni za kiimani.
Kwa niaba ya watumishi wakili wa Serikali Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Wakili Salehe Hassan amemshukuru mwezeshaji kwa mafunzo hayo na kwamba watumishi wote watayafanyia kazi na kujiupusha na viashiria ili kutastawisha afya ya akili.
WATUMISHI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WAKIFUATILIA MAFUNZO
YA NAMNA YA KUPAMBANA CHA CHANGAMOTO ZA AFYA YA AKILI
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.