Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe Joseph Mkude akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga amewaagiza Wajumbe wa Kamati ya Afya Msingi kuwahamasisha wazazi na walezi wenye watoto wa umri wa miezi tisa hadi miaka mitano kufika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo yatakayoainishwa kuanzia tarehe 15-18 Februari, 2024 ili kupata chanjo ya Surua na Rubela. Agizo hilo limetolewa leo Februari 14,2024 wakati wa kikao cha maandalizi ya chanjo hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Kikao hicho kimejumuisha wajumbe wa Kamati ya Afya wa Msingi Wilaya ya Shinyanga.
Akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella, Mratibu wa chanjo wa Manispaa ya Shinyanga Bw.Ramadani Maneno, amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inatarajia kutoa chanjo ya Surua na Rubella kwa watoto 69,352. Chanjo hiyo ina lengo la kuwakinga watoto wa miezi tisa hadi miaka mitano dhidi ya ugonjwa wa Surua na Rubella ambao huenea kwa njia ya hewa. Magonjwa ya Surua na Rubella huwa na dalili kuwa na vipele vidogo vidogo ambavyo huanza kwenye paji la uso na kusambaa sehemu zingine za mwili, kuchemka mwili , kukohoa na dalili ya macho mekundu huongezeka kwa mwenye ugonjwa wa Rubella.
Utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella kwa watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka mitano ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuwakinga watoto hao na magonjwa tajwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe Joseph Mkude, akimwakilisha Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga wakati wa kikao cha maandalizi ya chanjo ya Surua na
Rubella kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga.
Katibu wa Kamati ya Afya ya Msingi Dr.Nuru Yunge wakati wa kikao cha
maandalizi ya Chanjo
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Shinyanga
wakisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha maandalizi ya chanjo ya
Surua na Rubella
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.