Shirika la World Vision likishirikiana na Shirika la Kivulini wamegawa vitendea kazi kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii CHW katika Kata ya Samuye Halmshauri ya Wilaya ya Shinyanga,ili kuweza kuwarahishia utoaji huduma kwa wananchi .
Ndg, Shukrani Banyiezako Meneja wa world vision na Bi Eunice Mayengela wa Kivulini waliweza kugawa Baiskeli, tisheti, kofia, na begi vifaa vyote vikilenga kurahisiha ufikiwaji wa kila mhitaji hali kadharika utunzaji wa nyaraka pamoja na urahisi wa kutambulika pindi wakiwa katika maeneno yao ya kazi.
Bi Monica Mpolosi ni Mtendaji kata ya Samuye amewataka kwenda kutimiza majukumu yao na kuwasihi kuto danganya katika utoaji wa taarifa kwani tayari wamekabidhiwa nyezo zitakazo rahisisha ufikaji na ukusanyaji wa taarifa.
Vilevile Bi Monica amewakumbusha wanapoenda kutimizaa majukumu yao wasisahau kuhamasisha wananchi katika kaya zao kuwa na choo bora cha kisasa lakini pia kuwakumbusha kuwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi.
Mwisho Mtendaji huyo amewashukuru viongozi hao kwa kuwakumbuka watoa huduma za Afya ngazi ya jamiii na kwamba wasiache kuendelea kuwashika mkono kwani kazi yao ni kubwa katika Jamii
WATOA HUDUMA ZA AFYA NGAZI YA JAMII WAKISIKILIZA MAELEKEZO KUTOKA
KWA WADAU.
BAISKELI KWA AJILI YA KUWAFIKIA WAHITAJI KWA URAHISI
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.