Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini Mhe. Edward Ngelela
amesema hawatawafumbia macho Watendaji ambao wanakwamisha miradi ya maendeleo kwa kuwa Rais anajitahidi
na anahangaika kutafuta fedha za maendeleo. Hayo ameyasema leo Juni 14 , 2024 wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya
Hamashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari hadi
Juni, 2024 iliyowasilishwa kwa Kamati Kuu ya CCM Shinyanga Vijijini katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro amesema hatasita kuwachullia hatua watendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga ambao wanakwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kisingizio cha hatua za manunuzi
zisizofuata Sheria na weledi katika kazi. "........ fedha zinatengwa zinafika na zinatumwa kule zinapopaswa kwenda, watu wakiandika
madokezo wanaambiwa madokezo bado pesa zinaendelea kukaa, ......Mhe.Mwenyekiti huko nilikotoka hakuna fedha ilitengwa na
ikarudi Hazina, ikitokea hapa, nitakamata kila mtu na nitafanya vurugu kubwa na hakutakalika. Kama Mbunge amepambana na
Dr. Samia akazileta hairudi hata senti tano....” Amesisitiza Wakili Mtatiro
Kwa upande wao, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya wamempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.
Wajumbe hao wamewataka Watendaji kutekeleza miradi kwa wakati ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo .
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.