Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga , Wakili Julius Mtatiro amewataka Watendaji wa vijiji Kata ya
Solwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi kila robo.
Agizo hilo amelitoa wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua
kero za wananchi uliofanyika katika eneo la standi ya mabasi Solwa Juni 04 , 2024 baada ya
wananchi kuwasilisha malalamiko ya kutosomewa mapato na matumizi.
Wakili Mtatiro amebainisha kuwa usomaji wa mapato na matumizi ni wajibu wa kila Mtendaji ili
kuwawezesha wananchi kujua mafanikio na changamoto za maeneo yao.
“........nawaagiza Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji muanze kuwasomea wananchi mapato na
matumizi ili kuepusha migogoro na migongano hasa kwenyeutekelezaji wa miradi ya
maendeleo......”amesema Mtatiro.
Akiwasilisha salamu za kata , Diwani wa Kata ya Solwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha ambazo
zimetumika kutekeleza miradi ya maedeleo katika kata hiyo. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja
na ujenzi wa Zahanati, mradi wa umeme na maji katika kijiji cha Mwakatola, mradi wa maji na
ujenzi wa shule ya Sekondari katika kijiji cha Manigana, mradi wa vyumba vitatu vya madarasa
katika shule ya msingi Manigani, Solwa na Kashishi na mradi wa umeme na maji ya ziwa victoria
katika kijiji cha Mwabuki.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga amekuwa na ratiba ya mikutano ya hadahra kwa kila kata kwa ajili ya
kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.