Pikipiki hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndg David Rwazo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Ndg. Rwazo amesema lengo la kugawa pikipiki ni kuwasaidia Watendaji kuweza kufanya kazi zao ikiwa ni pamoja kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo na kusaidia shughuli za ukusanyaji wa mapato katika kata zao.
Aidha, amewasisitiza kuzitunza pikipiki hizo na zitumike katika kazi za Serikali na wasizigeuza kuwa chombo cha kufanyia biashara kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Maafisa Watendaji wa Kata waliopata pikipiki hizo ni Bi. Joyce Mahina wa kata ya Lyamidati, Bw. Majahasi Jakson wa kata ya Lyabusalu pamoja na Bi. Mary Shausi wa kata ya Tinde.
MKUU WA DIVISHENI YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU
NDG DAVID RWAZO AKIMPA PONGEZI MTENDAJI KATA YA LYAMIDATI BI JOYCE MAHINA.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.