Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ameendesha semina elekezi kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya Halmashauri, Kata na Kijiji Leo Septemba 30,2024 katika Ukumbi wa Halmashauri.
Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Ndg Joseph Ntomela amesema lengo la semina hii ni kuwafahamisha kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuwajengea uwezo wa kusimamia Uchaguzi.
Akifafanua kanuni hizo Wakili wa Serikali ambaye pia ni msimamizi msaidizi ngazi ya Wilaya Wakili Salehe Hassan amewataka kutekeleza kazi zao kwa kuzingatia taratibu na kanuni na kwamba kutenda kosa lolote kinyume na kanuni itapelekea kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Wakili Salehe alikazia juu ya kanuni inayowasimamia watu wenye mahitaji maalumu na namna wanavoweza kushiriki ipasavyo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Afisa Uchanguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg Oscar Lupavila aliwakumbusha juu ya sifa za mgombea, mpiga kura, pamoja na nafasi zitakazo gombewa kuwa ni Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Kijiji kundi mchanganyiko pamoja na Wajumbe wa Kijiji kundi la Wanawake.
"Tofauti na miaka ya nyuma Sasa hivi utaratibu umebadilika hatakuwepo Tena mgombea wa Kupitia bila kupingwa bali kutakuwepo na mgombea pekee ambapo Wananchi watapata haki ya kupiga kura ya ndio ama hapana" Ndg Lupavila aliongeza
Akifunga semina kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Ndg Ntomela weledi wao ndio utaenda kukamilisha Uchaguzi huru na Haki na kwamba waende kutekeleza majukumu yako kwa mujibu wa taratibu na kanuni walizopewa.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.