Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea na utoaji wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV) kwa mabinti wa miaka tisa hadi kumi na nne ili kuwakinga na vimelea vya ugojwa huo. Chanjo hiyo imeanza kutolewa katika maeneo mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuanzaia jana April 22, 2024 na zoezi hilo litamalizika tarehe 28 April, 2024. Maeneo hayo ni pamoja na mashuleni, vituo vya afya, zanahani na maeneo yaliyotengwa. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inatarajia kuwafikia Wasichana 42479 wenye umri wa miaka 9 hadi 14 na kuwapatia chanjo hiyo.
Akizungumzia umuhimu wa chanjo hiyo, Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Mwatanga Shaaban amewaasa wazazi kuwaruhusu mabinti zao kupata chanjo ili kujikinga na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Muuguzi wa Zahanati ya Solwa, Magoke Abeid akitoa chanjo ya kuzuai
Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Solwa
Kata ya Solwa.
Wasichana kutoka Shule ya Msingi Mawemilu wakionyesha kadi zao mara
baada ya kupata chanjo
Mganga wa Zahanati ya Mwakitolyo Dr. Festo Mzee akiwa katika picha ya
pamoja na Wasichana waliopata chanjo
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.