Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya halmashauri , Bi Monica Mnanka ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura ili wawe na sifa ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Wito huo ameutoa leo Oktoba 10, 2024 kwenye kipindi cha kuelimisha umma na kuhamasisha wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kupitia redio Faraja.
Akitaja sifa za mwananchi atakayeandikishwa, Bi. Mnanka amesema kuwa mwananchi atakayeandikishwa ni raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi, mkazi wa kitogoji husika na awe na akili timamu.
Aidha, amesema kuwa uandikishaji wa wapiga kura utaanza kesho tarehe 11 hadi 20 Novemba, 2024 katika vituo ambavyo vimeainishwa katika kila kitongoji. Vituo vya kuandikisha wapiga kura vitafunguliwa saa 2.00 Asubuhi na vitafungwa saa 12.00 Jioni.
Bi. Mnanka pia amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inatarajia kuandikisha jumla ya wapiga kura 236,621 kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.