Msimamizi Msaidizi ngazi ya Halmashauri Bw. Joseph Ntomela akiambatana na Msimamizi Msaidizi ngazi ya Kata ya Iselamagazi Bw. Amos Chacha leo Oktoba 13, 2024 wametoa elimu ya mpiga kura kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga waliofika katika mnada wa Iselamagazi.
Wasimamizi hao wametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura ili waweze kupata nafasi ya kushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba , 2024.
Bw. Ntomela amewakumbusha wananchi kuwa kuna utofauti baina ya uandikishaji unaoendelea ulioanza tarehe 11 hadi 20 Novemba, 2024 wenye lengo la kumwezesha mwananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uandishishaji uliopita ambao wananchi walipewa kitambulisho cha mpiga kura.
“Mwananchi tusichanganye, kuna wanaodai wameshajiandikisha na wana vitambulisho vya kupigia kura, uandikishaji huu unaoendelea ni kwa ajili ya kuchagua mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na wajumbe wa Serikali ya kijiji tarehe 27 Novemba, 2024, hivyo tujitokeze tukajiandikishe ili tuwapigie kura viongozi wetu” alisisistiza Ntomela
Utoaji wa elimu ya mpiga kura kwenye minada ni moja ya njia za mawasiliano ambazo halmashauri imejiwekea ya kuwafikia
wananchi wake ili waweze kupata elimu itakayowawezesha kushiriki vyema kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.