Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wananchi kutumia elimu kama silaa ya ukombozi wa maendeleo.
Amesema hayo wakati akifungua maadhimisho ya juma la wiki ya Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya stendi ya mabasi Iselemagazi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Oktoba 03, 2024.
Mhe. Mtatiro pia amewataka wazazi na walezi wa Mkoa wa Shinyanga kusimamia maadili ya watoto na vijana kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wanapata elimu bora na kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto na vijana shuleni na Nyumbani.
" mzazi atakae sababisha kukatishwa masomo kwa mtoto wake atachukuliwa hatua" amesema Mhe. Mtatiro
Aidha, Amewapongeza wazazi na walezi waliotoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha vijana wao wanaenda shule wakiwemo wasichana waliokatishwa masomo wamerejea tena shuleni kuendelea na masomo ili watimize ndoto zao.
Aidha, Mhe. Wakili Mtatiro alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kushiriki zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba, 2024
Wakati wa maadhimisho hayo, Mgeni Rasmi alipata fursa ya kutembelea banda ya Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga na taasisi mbalimbali.
“UJUMUISHI KATIKA ELIMU BILA UKOMO KWA UJUZI, USTAHIMILIVU, AMANI NA MAENDELEO”
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.