Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imepokea vifaa kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule za Msingi wenye Mahitaji Maalumu kutoka mashirika yasio ya kiserikali Action on Disability and Development (ADD) na Tanzania Cheshire Foundation ( TCF).
Alizungumza wakati wa mapokezi ya vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Kisena Mabuba amewashukuru wadau hao kwa kutoa vifaa hivyo kwa watoto wenye mahitaji maalum maana vifaa hivyo vinaenda kutengeneza maisha yao.
Aidha, Ndg, Mabuba amewapongeza wazazi wa watoto hao kwa kuwapeleka watoto shule wapate elimu bila kujali hali walizonazo.
“Kuna changamoto kubwa kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu , bado wanafungia watoto wao majumbani. Serikali tunaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya janga hili. Niendelee kusisitiza na wapongeza sana Wazazi kwa kuwaleta Watoto shule maana elimu ndio ufunguo wa maisha” alisema Ndg. Mabuba
Ndg Mabuba ametumia fursa hiyo kuwaeleza wazazi na wananchi kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bweni la Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Iselamagazi wenye thamani Shilingi 128,000,000, na kusema lengo la Serikali ni kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wananapata elimu bora na katika mazingira mazuri.
Awali, Afisa Elimu Maalum Awali na Msingi, Mwl. Irene Matern Kisweka akiwasilisha taarifa ya mapokezi ya vifaa hivyo amesema Halmashauri imepokea Viti Mwendo (Wheel Chair) 10 na Miwani 9 kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule za Msingi ambazo ni Iselamgazi, Pandagichiza, Mwalukwa A, Mwalukwa B, Mwamadilanha, Isela, Bunonga na Ng’hama.
Naye Ndg. Mabuba wakati akipokea vifaa hivyo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi inayowanufaisha watoto wenye mahitaji maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na sehemu mbalimbali za Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba
akizungumza wakati wa mapokezi ya vifaa
Mkurugenzi Mtendaji akipokea Kiti Mwendo kutoka kwa viongozi wa
Action on Disability and Development (ADD) na Tanzania Cheshire Foundation ( TCF).
Afisa Elimu Maalum Awali na Msingi, Mwl. Irene Matern Kisweka akiwasilisha taarifa
ya mapokezi ya vifaa.
Ndg. Mabuba akikabidhi Kiti Mwendo kwa Mwanafunzi pamoja na mzazi wake
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.