Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri Bw. Dhulkifl Sungura na Bw. Damian Ndassa wametoa wito kwa wanafunzi wenye sifa kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura ili wawe na sifa za kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti leo Oktoba 11, 2024 kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iselemagazi na Shule ya Sekondari Lyabusalu wakati wakitoa elimu ya mpiga kura kuhusu zoezi la uandikishaji wa wapiga kura na kuwahamasisha wale wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari.
Wakitaja sifa za mwananchi atakayeandikishwa, wamesema kuwa mwananchi atakayeandikishwa ni raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi, mkazi wa kitogoji husika na awe na akili timamu.
Wasimamizi wasaidizi hao wamesema kundi la wanafunzi ni kundi muhimu sana katika zoezi la kuandikisha wapiga kura kwa kuwa ndimo linapotoka kundi la wapiga kura wapya wanaopiga kura kwa mara ya kwanza. Hivyo, wanatakiwa kuelimishwa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia zoezi la uandikishaji na kuhamasishwa ili waweze kutumia haki yao ya kikatiba kujiandikisha na kuchagua viongozi wanaowataka.
Zoezi la kuandikishaji wa wapiga kura limeanza leo tarehe 11 hadi 20 Novemba, 2024 katika vituo ambavyo vimeainishwa katika kila kitongoji. Vituo vya kuandikisha wapiga kura vitafunguliwa saa 2.00 Asubuhi na vitafungwa saa 12.00 Jioni.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.