Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Bw. Andrew A. Mitumba, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amewapongeza washiriki wote waliofanya vizuri katika michezo mbalimbali nakuwataka kuiwakilisha vyema halmashauri katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa yatakayofanyika Mei 30 hadi Juni 2, 2024.
Hayo ameyasemaleo Mei 27, 2024 wakati wakufunga mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya halmashauri yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Iselamagazi. Mashindano hayo yalianza Mei 26 nakumalizika Mei 27, 2024.
“…. Wote mmejituma nakufanya kazi inayoonekana, wenzetu mliopatanafasi kwaniaba yetu sote tume wapa dhamana ya kubeba halmashauri yetu. Kwa kuwa mmeaminiwa nammefanya vizuri, huko mkajitume zaidi, mkacheze kufa nakupona huko tunataka vikombe. Lakini michezo inaendana na nidhamu, mkawe na nidhamu bora, mkawe wasikivu, hatutaki watoto wazururaji, ukigundulika unatabia za ajabu ajabu tutakuodoa mara moja…...” amesisitiza Bw. Mitumba.
Naye Kaimu Mkuuwa Kitengo cha Michezo Sanaa na Utamaduni Bw. Joseph Bihemo amesema kuwa team ya Halmashauri itawakilishwa na wanafunzi 110 ambao watashiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wakikapu, riadha, ngoma, kwaya na kuruka Kamba. Team hiyo itaambatana na makocha wanane.
Kauli mbiu ya michezo ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2024 ni “Miaka 50 ya UMITASHUMTA, tunajivunia mafanikio katika sekta ya Elimu, Michezo na Sanaa, Hima mtanzania Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024”
Wanafunzi 110 wanaounda timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na
Makocha nane watakaoiwakilisha halmashauri katika mashindano ya
UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa.
Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Bw.Andrew A. Mitumba,
Mwakilishiwa Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri yaWilaya ya Shinyanga
akifunga mashindano.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo, Sanaa na Utamaduni Bw. Joseph
Bihemo akitoa neono la utangulizi.
Wanafunzi wakiwa katika michezo mbalimbali
Baadhi ya wanafunzi na walioshiriki mashindano ya michezo
Makocha watakao iwakilisha halmashauri
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.