Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Wakili Julius Mtatiro amepiga marufuku walimu katika shule za msingi na sekondari kulima kwenye mashamba ya shule ili mashamba hayo yatumike kwa ajili ya kulimwa chakula cha wanafunzi.
Maagizo hayo ameyatoa leo Novemba 5, 2024 wakati akitoa salamu za viongozi katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025
Marufuku ya kulima mashamba ya shule imetolewa kufuatia hoja ambayo iliibuliwa na Diwani wa Nyida Seleman Segeleti, juu ya Walimu kuendelea kulima kwenye mashamba ya shule na wakati walizuiwa.
Mtatiro amesema Walimu hawazuiwi kufanya shughuli za kilimo kama sehemu ya kujiongeza kipato na kupata chakula, lakini suala la kulima kwenye mashamba ya shule hairuhusiwi, bali wanapaswa kukodi mashamba kwa wanakijiji na kufanya shughuli hizo.
“Mshamba ya shule yatumike kwa shughuli za shule ili wanafunzi wapate chakula, na siyo Walimu kulima Mashamba hayo,”amesisitiza Mtatiro.
Ameeleza kuwa Walimu kuendelea kulima kwenye mashamba ya shule, ni kuleta Mgogoro kwa jamii ambayo ipo tayari kulima mashamba hayo ili watoto wao wapate chakula shuleni, sababu wengine uwezo wa kuchangia chakula hawana, na kwamba tatizo hilo lilishatokea Manyada ambapo wazazi waligoma kuchagia chakula kutokana na mashamba ya shule kulimwa na Walimu, na wakati wao walikuwa wapo tayari kwenda kuyalima.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akizungumzia tatizo hilo, amemuangiza Mkurugenzi kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata wawaandikie barua walimu kwa kuambatanisha Waraka wa kuzuia Walimu kulima kwenye mashamba ya shule na kusambazwa kwa shule zote ili kumaliza tatizo hilo.
Mdhibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joyce Andrew, awali akijibu maswali ya Madiwani, amesema kwamba Waraka wa Walimu kuzuiwa kulima kwenye mashamba ya shule walishapewa na kusambazwa kwenye Kata zote.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.