Mradi wa Viazi Lishe"Forgotten Crops Project" unatekelezwa na shirika la " International Potato Center "(CIP) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga .Mradi huu unatekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri na shirika la CIP chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID), kupitia kituo cha utafiti "Agriculture Research Institute".
Mradi wa viazi lishe unalenga kuboresha lishe ya watoto chini ya umri wa miaka 5 kupitia viazi lishe ,ambavyo tafiti zinaonesha vina wingi wa Vitamin A ambavyo ni muhimu sana kwa afya ya akili na ukuaji wa mtoto na kuwakinga na maradhi mbalimbali.Pia mradi unalenga kutengeneza fursa za ujasiliamali kwa wakulima, kupitia uzalishaji wa ziada wa viazi lishe ambavyo hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za kusindika kama maandazi ,juisi,chapati ,kaukau(crips),tambi,michembe,na matobolwa ambapo mkulima anaweza kuongeza kipato chake kupitia ujasiliamali huo.
Mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miezi (18) ambapo kwa sasa upo kwenye mwezi wa 7 wa utekelezaji wake.
Katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mradi unafanya kazi katika vijiji 15 ambavyo ni sayu ,pandagichiza,kadoto B, Ng`hama,shatimba,mwampangabule,mwamakaranga,mwabundala,iselamagazi,lyabusalu,mwasingu,mwashilugulu,sumbigu na bukene.
Afisa lishe wilaya bw.Mankiligo said akielezea umuhimu wa viazi lishe kwa ukuaji wa afya ya mwili na akili kwa watoto.
Malengo ya mradi wa viazi lishe kwa wakulima wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ni pamoja na :
Mradi umetekeleza shughuli mbalimbali katika wilaya zikiwemo:
Kupitia mradi wa viazi lishe mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwemo:
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.