Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho ya kilele cha sikukuu ya Nane Nane kanda ya ziwa mashariki amewahimiza wakulima kufanya kilimo chenye tija na kutumia njia sahihi za kilimo bora ili kujipatia mazao bora na yenye thamani .
Ameyasema hayo Agosti 8,2024 wakati akizungumza kwenye kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane kanda ya Ziwa mashariki, maonyesho yaliyowakutanisha wakulima, wataalam wa kilimo na ufugaji kutoka Mikoa mitatu Shinyanga Mara na Simiyu yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Baridi Mkoani Simiyu na kuwataka wakulima kuachana na kilimo cha kubahatisha.
" kilimo cha kubahatisha kimepitwa na wakati hebu tubadilike wakulima, Shughuli za kilimo na ufugaji zikiendeshwa vizuri zinatija katika sekta ya kilimo, mafunzo haya na semina hizi tulizopata tangu tarehe 01 Agosti hadi leo kutoka kwa wataalamu wa kilimo na ufugaji hebu twendeni tukazitumie kwa usahihi.” amesema Mhe Mtambi
Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwembo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Kalekwa Kasanga.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mtambi amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuchagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa uwepo wa maonesho haya kwa kanda ya Ziwa Mashariki ni fursa kubwa sana kwa wananchi wa Mikoa hii mitatu ya Shinyanga , Mara na Simiyu kwani imekutanisha wataalam wa Serikali, Taasisi na Sekta binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi ambaye alikuwa mgeni
rasmi akizungumza wakati wa maadhimisho.
Mkurugenzi wa Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Dkt. Kalekwa Kasanga alipotembelea Banda la halimashauri.
Picha ya pamoja ya mgeni rasimi Mhe. Kanali Evans Mtambi ambaye ni
Mkuu wa Mkoa wa Mara pampja na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mhe. Anamringi Macha na mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.