Hayo yameelezwa na Dkt. Charles Zakaria kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakati akizungumzia ujio wa madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na watoto ambao wameanza kutoa huduma za kibingwa hospitalini hapo kuanzia Oktoba 14 2024 na huduma hizo zitatamatika Oktoba 18, 2024.
Akielezea kuhusu huduma za kibingwa zinazotolewa hospitalini hapo, Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Dkt. Mwita Chacha amesema lengo la kutoa huduma hizo ni kuwapunguzia wananchi changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma na kuwajengea uwezo madaktari wenyeji.
Aidha, Dkt Mwita ameainisha magonjwa ambayo wanakutana nayo wakati wa kutoa huduma kuwa ni matatizo ya figo, shida katika mfumo wa hewa na matatizo ya njia za kupitisha damu ambapo kuna kifaa maalumu cha kupima moyo ambacho kinapatikana hospital ya halmashauri.
“kwa matatizo ya moyo kwa watoto tukiyaongelea yapo mengi kuna yale ya kuzaliwa na tundu la moyo, wengine wanazaliwa na moyo mkubwa lakini mtoto anaweza kuvamiwa na wadudu kwnye koo na kusababisha madhara kwenye moyo” aliongeza
Akitoa shukrani kwa niaba ya waliopata matibabu ya kibingwa mama wa mtoto aliyezaliwa njiti Bi. Shose Exaud Mosha amewashukuru madaktari kwa kumsaidia kumhudumia mtoto wake na kuwashauri kina mama wenye watoto wawalete kupata huduma.
Awali, Dkt Charles amefafanua kuhusu gharama za matibabu amesema huduma hizo zitatolewa kwa utaratibu wa kawaida kwa mwananchi wenye bima hali kadharika mwenye pesa taslimu.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.