Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashjauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndg. Kisena Mabuba ametoa maagizo hayo katika Kikao kazi cha kupitia na kujadili takwimu za utendaji wa huduma za Afya na taarifa ya mapato na matumizi katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kubaini changamoto na kuweka mpago kazi wa kuongeza mapato katika vituo hivyo.
Kikao hicho kimefanyika Mei 16,2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na kuhudhuliwa na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa pamoja na Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza katika Kikao hicho, Ndg. Mabuba amewataka Waganga Wafawidhi kutoa huduma bora kwa kuzingatia Weledi, Taratibu, Kanuni za Utumishi wa Umma.
“Watumishi wenzangu zingatieni Taratibu, Kanuni za Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yenu, mkakusanye mapato kwa uwaminifu na kuboresha huduma katika vituo vyenu vya kazi” alisema Ndg.Mabuba.
Mkurugenzi Mtendaji amemuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga kuandaa mafunzo ya kuwajengea na kuwaongezea uwezo Wataalam wa Afya katika matumizi ya Mifumo ya mapato ili kupunguza vikwazo vya ukusanyaji mapato
.
Amempongeza Mgaganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mwajiji kwa ukusanyaji mzuri wa mapato na kuvuka lengo na kuwataka Wataalam kujifunza kupitia Zahanati ya Mwajiji ili kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Aidha, Ndg. Mabuba amesisitiza matumizi ya lugha nzuri kwa Wagonjwa na kuwahimiza Wataalam hao kuzingatia usafi wa Mazingira katika Vituo vya kutolea huduma za afya.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri amewataka Wagaganga Wafawidhi kutekeleza maagizo yaliotolewa ili kuongeza ukusanyaji mapato na kuahidi kusimamia utekelezaji huo.
Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Kisena Mabuba akizungumza wakati wa kikao na
waganga Wafawidhi
Mganga Mfawidhi akichangia Mada wakati wa kikao
Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kulolea huduma ya Afya Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwenye picha ya
pamoja na Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.