Wafugaji Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wametakiwa kutumia majosho kuogesha mifugo yao ikiwa ni njia ya kuzuia wadudu waharibifu na magonjwa ya mifugo ili kuwa na mifugo yenye afya bora. Kauli hiyo imetolewa leo Februari 20, 2024 na Mweyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Shinyanga Vijijini Ndg. Edward Ngelela wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleao inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sinyanga ukiwemo mradi wa ujenzi wa Josho la kuogeshea mifugo lililopo katika kata ya Solwa.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa josho hilo, Ndg. Ngelela amefafanua kuwa kuogesha mifugo kwa kutumia josho huua wadudu wote waharibifu na magonjwa yaa mifugo kwa kuwa mfugo huingia mwili mzima kwenye josho tofauti na uogeshaji wa kunyunyizia ambao huua wadudu kwa baadhi ya sehemu katika mwili wa mfugo.
Aidha, Ndg. Ngelela amemwagiza afisa mifugo kuhakikisha elimu juu ya umuhimu wa kuogesha mifugo kwa kutumia majoshi inatolewa kwa wafugaji kuwa na mifugo yenye afya.
Awali akiwasilisha taaarifa ya mradi huo, Afisa Mifugo wa Kata ya Solwa, Bw. Lukali Marick amesema mradi huo umekamilika na umegharimu kiasi cha Tsh. 23,000,000.00. Josho la Solwa limeanza kufanya kazi mwezi Desemba 2023 na linahudumia mifugo ya vijiji vinne ambavyo ni Solwa, Mwandutu, Mwasekage na Mwisemi. Mradi huo wa Josho unasimamiwa na Kamati ya Josho chini ya usimamizi wa Serikali ya Kijiji na umefanikiwa kuthibiti wadudu waharibifu na magonjwa ya mifugo.
Muonekano wa Josho lililijengwa na Serikali katika Kata ya Solwa
linalohudumia vijiji vinne katika kata hiyo.
Afisa Mifugo wa Kata ya Solwa, Bw. Lukali Marick akitoa taarifa ya Mradi
wa Josho la kuogeshea mifugo
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.