Timu ya Maafisa Biashara kutoka Divisheni ya Viwanda Biashara na Uwekezaji wakiongozwa na Afisa Biashara Bi. Gloria Allen Mwakyusa wametoa Elimu ya Ushuru wa Huduma kwa wafanyabiashara wa Kata ya Didia ikiwa ni muendelezo wa kutoa elimu katika kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Bi. Gloria amesema ni muhimu kutoa elimu hii kwa wafanyabiashara ili wakianza kuchangia wafahamu kuwa ni kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe katika kuboresha miundombinu itakayowezesha Biashara zao kustawi.
Ushuru wa Huduma unatozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa mfanyabiashara kwa huduma anazotoa kutokana na kutumia miundombinu ya Umma inayomwezesha kufanyabiashara na unasimamiwa na Sheria inayoratibu fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1983 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 pamoja na Sheria ndogo ndogo za Halmashauri.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.