Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na TACAIDS wakiambatana na Wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali yakiwemo PACT, TPHS na Fhi 360 Watembelea Kikundi cha Upendo kutoka Kata ya Samuye cha Mradi wa DREAMS unaotekelezwa na SHADEFA Septemba 23, 2024.
Kikundi cha upendo kinaundwa na wasichana wa lika kuanzia miaka 10 hadi 14 wamejengewa uwezo wa kijiamini , wameiva katika afua za mabadiliko ya tabia, huduma za kitabibu, na kiuchumi. Kikundi hiki ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa DREAMS.
Mradi wa DREAMS unalenga kupunguza maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi ( VVU) .
Aidha, wajumbe wa Kikundi cha Upendo wasisitizwa kuendelea kutumia kinga ( Condom) ili kulinda Afya zao.
Vilevile, Wasichana hao walihimizwa kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na halmashauri, pamoja na mabenki ili kukuza uchumi wao.
WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII PAMOJA NA TACAIDS
WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WANAKIKUNDI CHA DREAMS.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.