Ni katika warsha iliyokutanisha Halmashauri tatu ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Shinyanga Manispaa pamoja na Misungwi ambazo zinatekeleza mradi wa Elimu Jumuishi, Task Order 51.
Warsha hiyo imefayika katika hoteli ya Karena Shinyanga mjini ikiwa na lengo la uboreshaji wa mkakati wa ushirikishwaji wa mashirika ya watu wenye ulemavu.
Akizungumza katika warsha hiyo muwezeshaji Bi. Anasteria Gwajima ambaye ni mratibu wa maswala ya jinsia emeelezea namna ya kumsaidia mtu mwenye ulemavu wa macho kwamba ni vizuri unapomuongoza vyema ukamueleza kwa maneno mazingira unayotembea naye ikiwa kuna shimo, kona ama ngazi na sio kumvuta mkono.
Bi Gwajima ameongeza kuwa si vyema wanaume kukimbia familia zao kwa kigezo cha kupata mtoto mwenye ulemavu huku akilaani wale wanaotumia majina kandamizi na kwamba ni vyema unapomtambulisha uanze na neno mtu mwenye ulemavu ili kutunza utu wake.
Akichangia namna ya kuhudumia watu wenye ulemavu Mwl, Moshi Bucheyeki Enos wa Shule ya Msingi Mwalukwa A amesema ni muhimu kuendelea kuomba wadau kutengeneza mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu ili kusaidia kundi hilo kuchanganyika na wengine.
Kwa upande wake Afisa Elimu Maalumu shule za Msingi Bi Irene Kisweko wa Shinyanga Dc amesema serikali inaendelea kumuangalia mtoto mwenye ulemavu kwa kuweka miundombinu wezeshi ikiwa ni pamoja na kumpatia chakula kumsaidia katika mazingira yake ya masomo.
Mradi wa Elimu Jumuishi unatekelezwa na umoja wa mashirika manne ADD International, Light for the World, Sense International na Tanzania Cheshire Fondation ukikutanisha mashirika ya watu wenye ulemavu pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali.
BAADHI YA WASHIRIKI WA WARSHA KWENYE KAZI ZA MAKUNDI.
MWL MOSHI BUCHEYEKI WA SHULE YA MSINGI MWALUKWA AKITOA MCHANGO WAKE.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.