Ni katika mafunzo ya waandishi na waandaji wa orodha ya wapiga kura yaliyofanyika Leo Oktoba 8, 2024 katika vituo viwili vya Didia na Iselemagazi.
Akitoa mafunzo hayo Msimamizi Msaidizi ngazi ya Halmashauri Ndg Damian Ndassa amewataka waandishi hao kuandikisha watu wenye sifa stahiki.
Akibainisha sifa hizo Ndg Ndassa amesema ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania, umri wa zaidi ya miaka kumi na nane, akili timamu pamoja na kuwa mkaazi wa Kitongoji husika.
Mapema kabla ya kuanza mafunzo waandishi hao walikula kiapo Cha utii na kutunza siri kilichotolewa na Hakimu mkaazi Mahakama ya Tinde, Hakimu Doris Mgonja ambaye aliwataka kutunza kiapo chao.
Mafunzo hayo yamejumuisha Kata 15 ikiwemo Lyamidati, Usule, Imesela, Bukene Didia Puni Nyida na itwangi waliofanyia ukumbi wa Shule ya Msingi O.L.A pamoja na Kata za Iselamagazi, Lyabusalu, Mwantimi, Pandakichiza, Nyamalogo na Mwalukwa waliofanyia Ukumbi mpya wa Halmashauri.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.