Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imetoa mafunzo kwa Waandishi na Waandaji wa orodha ya Wapiga Kura watakaotekeleza zoezi la uandikishaji wapiga kura linalotarajia kuanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.
Mafunzo hayo ambayo yamepangwa kufanyika kwa siku mbili katika kanda nne yameanza leo Oktoba 07, 2024 kwa kuhusisha kanda mbili zenye washiriki kutok kata 11 za Kata ya Tinde, Nsalala, Usanda, Masengwa, Mwamala, Samuye, Mwenge, Salawe, Solwa, Mwakitolyo na Lyabukandena yamefanyika katika kumbi za shule ya Sekondari ya Wasichana Tinde na Shule ya Sekondari Nzuzuli.
Kabla ya kuanza kwa mafunzo, waandishi na waandaaji wa orodha ya wapiga kura wamekula kiapo cha uaminifu, uadilifu na kutunza siri.
Wakifungua mafunzo kwa niaba ya Msimamizi wa uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi 2024 ngazi ya halmashauri Ndg. Victor Mollel na Bi Monica L. Mnanka wamewataka
waandishi na Waandaaji wa Orodha ya wapiga kura kuzingatia Sheria, Kanuni , miongozo na maelekezo ya Serikali katika zoezi hilo ili kufikia lengo la kuandikisha watu wote wenye sifa za mipiga kura.
Aidha, amewataka Waandishi na waandaaji wa Orodha ya Wapiga kura kusikiliza kwa makini wakati wawezeshaji wakiwasilisha mada mbalimbali kuhusu zoezi la uandikishaji ili waweze kufahamu utaratibu wa kuandikishaji wa wapiga kura.
"Msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri hategemei kusikia mtu ameharibu kazi kwa uzembe wake na badala yake kazi ikamilike vizuri kwa mujibu wa sheria za nchi" wamesisitiza .
Naye mwezeshji wa mafunzo ambaye ni Afisa Uchaguzi, Ndg. Osca Lupavila amesasilisha mada kuhusu utaratibu wa uandikishaji, sifa za anayeandikishwa, mawakala wa vyama vya siasa n utunzaji wa vifaa.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.