Kuelekea Uchaguzi was Serikali za Mitaa Novemba 27,2024 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa Elimu kwa Vyama vya Siasa kuhusu Sheria, Taratibu na kanuni za Uchaguzi leo Oktoba 22,2024.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Ndg. Frank Shija amesema katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Msajili wa Vyama vya Siasa anaviasa vyama vya siasa kuzingatia Sheria za nchi zikiwemo Sheria za Uchaguzi na Sheria zote zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinazohusika katika uchaguzi huo, ili kudumisha Ushiriki wa Uchaguzi ambao ni jukumu la msingi la chama cha siasa, Uhusiano mzuri baina ya wadau, Utii wa Sheria bila shuruti, Uvumilivu wa kisiasa na Amani, utulivu, uzalendo, muungano wa Tanzania na Umoja wa kitaifa uliopo katika nchi yetu.
"Vyama vya Siasa vina wa wajibu wa kufuata wakati wa uchaguzi; Kuheshimu sheria zinazosimamia uchaguzi pamoja na kuzingatia pamoja na kuzingatia kanuni za maadili ya vyama vya siasa na kanuni za kuratibu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kulaani , kuepuka na kuchukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu, kutotoa maneno au maandishi ya uongo dhidi ya mtu au chama cha siasa kingine, kujiepusha na vitendo vya rushwana na kujiepusha na vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote" amesema Ndg. Shija
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Kalekwa Kasanga amewashukuru Viongozi hao wa vyama vya siasa kwa namna ambavyo wameonesha ushirikiano wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura na kuomba kuendelea kutoa ushirikiano kwa matukio yaliosalia kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.