Mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) (FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) yameanza leo katika hoteli ya Vigmark mjini Shinyanga.
Zaidi ya washiriki 60 katika makundi ya waratibu elimu kata katika kata zote za Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, mkuu wa kituo cha afya na mhasibu wa kila hospitali ya wilaya wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa FFARS katika vituo vya kutolea huduma zikiwemo zahanati, vituo vya afya, hospitali na shule za msingi na sekondari.
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha washiriki hao ili waweze kuufahamu mfumo na kuweza kwenda kutoa mafunzo ya utumiaji wa mfumo wa FFARS kwa watoa huduma waliopo katika ngazi za shule za msingi na sekondari, na vituo vya afya wakiwemo kila mkuu wa kituo cha afya, mhasibu wa kila shule ya msingi na sekondari.
Mafunzo ya leo ni matokeo ya mafunzo yaliyofanyika tarehe 5 hadi 6 Juni 2017 ambapo wahasibu zaidi ya 130 kutoka Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati walipatiwa mafunzo ya Mfumo wa FFARS ambao kwa leo wamekuwa wawezeshaji kwa washiriki zaidi ya 60 waliohudhuria mafunzo. Wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3, TAMISEMI, Wizara ya afya kupitia HPSS (Health Promotion and System Strengthening) na Wizara ya Elimu wameshiriki katika kutoa mafunzo kwa kuhakikisha mafunzo yanaendeshwa kwa ufanisi wenye matokeo chanya.
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dr. Suma Kaare, alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma utasaidia kurahisisha kazi na tayari serikali imeukubali na utaanza kutumika kuanzia mwezi Julai, 2017 katika halmashauri mbalimbali.
Baada ya mafunzo haya, wahitimu wataenda kutoa mafunzo katika vituo vya kazi vinavyotoa huduma kuanzia tarehe 19 hadi 30 Juni 2017
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.