Mradi wa ujenzi wa tanki la maji kutoka Ziwa Victoria katika kijiji cha Mwalukwa ambao unahudumia vijiji vinne vya Mwalukwa, Bulambila, Kadoto na Ng'hama umeziduliwa jana Agosti 12, 2024 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Godfrey Mnzava.
Mnzava amewapongeza washirika wa maendeleo kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazowaikabili jamii na ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kuendelea kuwa na uhakika wa kupata maji.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi, Mkurugenzi wa Shirika la Life Water Internation Tanzania Ndg. Devocatus Kamara amesema huo mradi unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1,107,427,695 na umekelezwa na shilika hilo kwa kushirikiana na RUWASA na jamii
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.