Dkt. David Mosses kwa niaba ya Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga amewashauri vijana kutumia fursa ya huduma za madaktari bingwa wa mama Samia kupima afya zao.
Wito huo ameutoa leo Novemba 06, 2024 wakati akitoa takwimu za wagonjwa wanaofika kupata huduma za kibingwa zinazotolewa na madaktari bingwa wa Mama Samia katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga zilizoanza kutolewa Novemba 04, 2024.
Dkt David amesema wananchi wamekuwa na mwitikio mzuri na wameendelea na kunufaika na huduma hiyo.
Aidha, Dkt. David amebainisha kuwa kundi la wazee ni kundi ambalo linaongoza kufika hospitalini hapo kupata huduma.
Naye kiongozi wa kundi la maktari bingwa wa wanaotoa huduma za kibingwa, Dkt. Rebecca Samwel ambaye ni Daktari bigwa wa usingizi amesema lengo ni kuwafikia na kuwapunguzia gharama na usumbufu wananchi wenye changamoto za kiafya kwani watapata huduma za kibingwa ambazo wangezipata kwa kusafiri kwenda hospitali kubwa kama Muhimbili na Bugando.
Dkt. Rebecca ameongeza kusema kuwa toka huduma zimeanza kutolewa wameshapokea wagonjwa wenye changamoto za matatizo ya uzazi kwa wanawake, shinikizo la damu, vidonda vya tumbo, Watoto wenye selimundu pamoja na utapiamlo.
Huduma zote zinatolewa kwa gharama nafuu. na huduma hizo zitatamatika Novemba 10, 2024
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.