Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. JOHARI SAMIZI leo tarehe 28.02.2023 amezindua rasmi kamati ya watu wenye ulemavu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Katika uzinduzi huo, ameelezea kuwa bado kuna changamoto ya ukatili, unyanyasaji, na unyanyapaa dhidi ya Watu wenye Ulemavu, lakini pia mila potofu zinazopelekea baadhi ya Watu wenye Ulemavu kufichwa kwa kufungiwa ndani na pia ukiukwaji wa haki za Watu wenye Ulemavu unaopelekea madhara makubwa kwa wahusika.
Ikumbukwe kuwa Mtu mwenye Ulemavu yupo kwenye hatari kubwa ya kunyimwa au kunyang’anywa haki zake ukilinganisha na Mtu asiye mlemavu. Hivyo basi, aliiomba kamati hiyo kuendelea kuwa watetezi wa masuala mbalimbali yanayowahusu watu wenye ulemavu .
Aidha, aliipongeza kamati hiyo na kueleza kuwa itaenda kuibua na kusaidia changamoto mbalimbali zinazowahusu watu wenye ulemavu.
Mwenyekiti wa kamati ya watu wenye ulemavu Bw. Moshi Enos aliwashukuru wadau wa shirika la ADD INTERNATIONAL- TANZANIA kwa kufanikisha kikao hicho .Aidha alieleza kuwa watu wenye ulemavu wana changamoto nyingi, hivyo ni muhimu kuendelea kushirikiana kwa pamoja kutoa elimu kwa jamii kutowaficha watoto wenye ulemavu.
Wajumbe wa kamati ya watu wenye ulemavu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.