Wanafunzi wa Shule ya Msingi Iselamagazi wakipata kifungua kinywa na chakula cha Mchana leo Machi 15, 2024. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inaendelea na utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ya chakula shuleni kwa shule za msingi ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa utoaji chakula shuleni uliozinduliwa na Serikali tarehe 16 Novemba, 2023.
Katika uzinduzi huo, Serikali ilitoa maelekezo kwa Sekretarieti za Mikoa, Serikali za Mitaa na Wadau mbalimbali kuwa kila ngazi ya utekelezaji wa usimamizi wa elimu msingi kuweka utaratibu wa kuandaa mpango kazi wa upatikanaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni.
Wakati wa uzinduzi, ilielezwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa chakula na lishe kwa mafanikio ya kitaaluma na ujenzi wa afya za wanafunzi kwa sababu mwanafunzi aliyeshiba darasani wakati wa masomo atakuwa na msikivu, mtulivu na mwenye kupenda shule wakati wote.
.
Baadhi ya Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kutoka Shule ya Msingi
Iselamagazi wakipata kifungua kinywa
Baaadhi ya wanafunzi wa darasa la sita na la saba kutoka Shule ya Msingi
Iselamagazi wakipata mlo wa mchana
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.