• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Government Web Framework
Government Web Framework

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwongozo wa Tovuti za Serikali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Maendeleo, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Usafi na Manzingira
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Nyuki na Misitu
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha na Mipango
      • Kamati ya Masuala ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Elimu , Afya na Maji
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
    • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
    • Madiwani wa Kuchaguliwa
    • Madiwani wa Kuteuliwa
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Majarida
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Kanzi Data ya Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Video

UMATI WAFURIKA KUMUAGA DIWANI KATA YA ITWANGI

Posted on: October 7th, 2024

Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga na Watumishi leo Oktoba 7, 2024 wamemsindikiza katika makazi yake ya kudumu aliyekuwa Diwani wa Kata ya Itwangi Mhe Sonya J Mhela ambaye amezikwa katika makabuli ya familia yaliyopo Kijiji Cha Itwangi.


Ibada ya kumuaga Mhe. Sonya imeongozwa na Mchungaji Richard Mashauri ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa la Adventista Wasabato Jimbo la Nyanza Gold Belt Field ametoa neno la faraja kwa familia kutoka kitabu cha Ayubu 14:1 ambalo linakumbusha mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi duniani si nyingi.


"umepewa uhuru wa kuchagua kuamini ama kumkataa Yesu kuwa bwana na mwokozi wetu na hakika watakao mchagua watafanyika wana na kwamba ibada  ya kumuaga ndugu yetu Sonya ni ibada ya sisi tuliobaki hai" aliongeza mchungaji Mashauri



Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,  Wakili Julius Mtatiro akitoa salamu za Mkoa na Wilaya amesema  siku ya kumpumzisha Marehemu Sonya imekuwa siku  ngumu kwa Kila mmoja na  asingeweza kuandaa  hotuba ndefu zaidi ya maneno ya faraja yaliyotolewa na viongozi wa kiroho .


"jambo la  muhimu ni kumuombea marehemu apumzishwe salama na kwamba funzo pekee ni kuendelea kutii maelekezo ya watumishi wa kiroho ikiwa ni kutenda matendo mema na kumcha Mungu"


Aidha Wakili Mtatiro ameongeza kuwa kuondoka kwa Diwani Sonya sio mwisho wa Serikali kutoa huduma katika kata ya Itwangi na kwamba yote yaliyoanzisha yatakamilishwa.



Naye Ndg. David Rwazo  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa

liofika kwenye msiba huo.


 Akimzungumzia marehemu wakati wa uhai wake  amesema atakumbukwa kwa  kuisimamia vyema  miradi ya maendeleo katika kata yake na halmashauri kwa ujumla.


Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Kata ya Itwangi Afisa elimu wa kata Ndg  Ashery essero Mafuru  amesema  kata imempoteza mpambanaji na kiongozi madhubuti  aliyeweza kumsaidia kila mwananchi hivyo wataendelea kuyaishi  na kuyaenzi maisha yake.


Wakati wa uhai wake Mheshimiwa Sonya Mhela alishika nyadhifa mbalimbali kama katibu wa wazazi kata ya Itwangi, mwenyekiti wa Kijiji Itwangi, mwenyekiti wa kamati ya uchumi ya Wilaya na mpaka umauti unamfika alikuwa Diwani wa Kata ya Itwangi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira.


Mheshimiwa Sonya alifariki Dunia Oktoba 4, 2024 katika Hospital ya Rufaa Bugando alikokuwa anapatiwa matibabu.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 09, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA ( MCHUJO) KADA YA DEREVA DARAJA LA II April 15, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA TATU April 17, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI April 19, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MITI 1000 YAPANDWA KATA YA SALAWE KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU.

    December 09, 2024
  • BABA BORA, SAUTI YA UMMA NA WANAWAKE VIONGOZI WAPATIWA VITENDEA KAZI

    November 15, 2024
  • WANADIDIA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI NOVEMBA 27, KUPIGA KURA

    November 15, 2024
  • MASHINE YA X-RAY MBIONI KUFIKA KITUO CHA AFYA TINDE

    November 15, 2024
  • Tazama zote

Video

wiki ya maji
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Muundo wa Taasisi
  • Muundo wa Taasisi
  • Video mbali mbali
  • Historia
  • Fomu ya Likizo
  • Leseni ya Makazi
  • Fomu ya Mkazi wa Ardhi kulipwa fidia

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • ofisi ya taifa ya takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Government Web Framework

Wasiliana nasi

    NIndo - Iselamagazi

    Anuani ya posta: 113 Shinyanga

    Simu: 0282-986382

    Simu: 0282-986382

    Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.