Kamati ya Fedha ,Uongozi na Mipango ilifanya ziara ya ukaguzi wa kawaida wa miradi ya maendeleo tarehe 19 oktoba , 2017 kuona hali halisi ya utekelezaji na fedha zilizopokelewa kutekeleza miradi hiyo.
Jumla ya miradi sita (06) ilitembelewa na kamati na kutoa maagizo na utekelezaji wake.
Kamati ya Fedha ,Uongozi na Mipango ikiwa inakagua mradi wa skimu ya umwagiliaji iliyopo katika kata ya Nyida kijiji cha Nyida wilayani Shinyanga.Kutoka upande wa kulia Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ngassa Mboje akisikiliza maelezo ya kitaalam kuhusiana mradi kutoka kwa mkuu wa idara ya kilimo Ndg. Edward Maduhu. Mradi huu umeghalimu kiasi cha Tshs.120,000,000 kati ya fedha hizo kiasi cha Tshs.20,000,000 ni michango kutoka kwa wananchi.
Kamati ya Fedha , Uongozi na Mipango ikiwa inakagua ujenzi wa josho katika kijiji cha Zobogo. Mradi huu wa josho la kuogeshea mifugo uliopo katika kata ya Itwangi kijiji cha Zobogo umekamilika na umeghalimu kiasi cha Tshs.20,000,000.
Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye kikao katika kata ya Nsalala kijiji cha nsalala wakiwa wanazungumza vikundi vya wakinamama waliopatiwa mikopo ya wanawake.
Baadhi ya vikundi vya kina mama waliopatiwa mikopo katika kata ya Nsalala wilayani Shinyanga.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.