Ujenzi wa vyumba 45 vya madarasa katika Shule 18 za sekondari zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga umeanza kutekelezwa ambapo wananchi wa maeneo husika, Madiwani, paoja na Management kushirikiana na mafundi wazawa (Force Account) wamejenga maboma ya majengo hayo na kwa sasa yako katika hatua za ukamilishwaji wa Maboma hayo ambayo yako hatua mbali mbali za Ujenzi.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hii hivi karibuni Mkuu wa idara ya ujenzi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhandisi William Luciu amesema kuwa ujenzi wa madarasa katika shule zote 18 ambazo zinatekeleza mradi huo umeshaanza ambapo umewashirikisha wananchi wa maeneo husika na kwa sehemu kubwa ujenzi wa hatua za maboma uko katika hatua za ukamilisha wa Maboma
Mhandisi Luciu ameeleza kuwa idara yake kwa kushirikiana na idara ya elimu Sekondari pmaoja na Walezi wa Kata na Management ya Halmshauri ya Wilaya ya Shiyanga wamejipanga kikamilifu katika usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi huo na kwamba watahakikisha ujenzi unakamilika ndani ya muda uliopangwa na kujenga madarasa yenye viwango vya hali ya juu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza 2023 kupata mahala pa kujifunzia.
Hivi Karibuni Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ilipokea jumla ya Shilingi 900,000( Millioni 900 ) kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 45 vya madarasa ambayo yatatumiwa na wanafunzi wanaotaraji kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 katika shule 18 zilizobainika kuwa na uhitaji Zaidi wa madarasa ya msingi. Mapema. akizipokea Pesa hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Dr. Nice R. Munissy, alimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuipatia Halamshauri na watu wa Shinyanga DC kiasi cha pesa hizo ili kuhakikisha watoto wote wanaochaguliwa kwenda shule Jan 2023 wasikose mahala pa kujifunzia.
Shule zilizopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 ni pamoja na Shule ya Sekondari Iselamagazi (2), Mishepo (1), Ng'wakitolyo (1), Solwa (8), Gembe (1), Salawe (5), Kituli (4), Tinde (2), Ihugi (2), Usule (3), Didia (4), Mwalukwa (2), Kaselya (1), Isela (1), Ilola (1), Lyabukande (3), Imenya (1) na Itwangi (1) ambapo kila chumba cha darasa kitajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 20.
Kwa Kusoma Taarifa ya Ujenzi wa Madarasa haya Mpaka tarehe 08.11.2022 tafadhali pakuwa Document ujenzi wa madarasa-Shy DC Mpaka 08.11.2022.pdf
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.