Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wametakiwa kujaza kwenye mfumo wa PEPMIS utekelezaji wa majukumu yao wanayoyafanya kila siku ikiwa ni utekelezaji wa matumizi ya mfumo huo ambao unalenga kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Upendo Sianga wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa mfumo wa huo wa kieletroniki wa usimamizi wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mei 21, 2024.
Naye Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Vaileth Lumeleziameelezea lengo la kufanya zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mfumo wa PEPMIS kuwa ni kubaini changamoto zinazowakabili watumishi katika utumiaji wa mfumo huo ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Mfumo wa PEPMIS ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambao ni mbalada wa mfumo wa OPRAS ulikuwa ikitumika kupima utendaji kazi wa watumishi wa umma
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bi. Upendo Sianga akielekeza namna ya kutumia mfumo wa PEPMIS
kwa watumishi.
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Vaileth Lumelezi akitoa
neno la utangulizi wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa mfumo wa PEPMIS
Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Halmasahuri ya Wilaya ya Shinyanga
Bi Jane D. Gwaharage akiwakisilisha tathmini ya utekelezaji wa matumizi ya
mfumo wa PEPMIS wa kila Divisheni na Kitengo.
Baadhi ya Watumishi kutka Halmasahuri ya Wilaya ya Shinyanga wakifuatilia
kwa makini wakati wa zoezi la ufuatiliaji w autekelezaji wa mfumo wa PEPMIS
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.