Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Nuru Yunge leo 19/03/2024 imetembelea Mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri lililopo Kata ya Iselamagazi.
Lengo la ziara hiyo ni kufanya tathimini ya mwenendo wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
Akizungumza katika ziara hiyo Dkt. Yunge amewataka wataalam kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano katika usimamizi wa mradi huo.
“ Tuendelee kusimamia Mradi kwa ushirikiano , nawaomba sana tufanye kazi kama timu, kila Mkuu wa Divisheni na kitengo atimize wajibu wake kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati” Amesema Dkt. Yunge.
Menejimeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ikikagua mradi wa ujenzi
wa jengo la utawala la Halmashauri.
Mwonekano wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.