Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Johari Samizi amewataka Watendaji Kata na Maafisa Elimu wa Halmashauri mbili za Wilaya ya Shinyanga kusimamia utekelezaji wa mpango wa chakula mashuleni ili kukuza kiwango cha ufaulu. Hayo ameysema wakati wa kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Disemba, 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Shinyanga Machi 01, 2024. Kikao hicho kimejumuisha watalaam kutoka ofisi ya Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya aya Shinyanga.
“ Kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya chakula na ufaulu wa masomo kwa watoto.Tafiti zinaonyesha watoto wanaopata chakula mashuleni wanafanya vizuri katika masomo, shirikisheni wazazi na tuendelee kutoa elimu kwa wazazi hao kuhusu umuhimu wa watoto kupata chakula mashuleni...” alisisitiza Mhe. Samizi.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Afisa Lishe wa halmasahuri hiyo, Bw. Said Mankligo amesema kuwa katika kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Disemba, 2023, halmashauri imefanya shughuli za usimamizi na utekelezaji wa mkataba wa Lishe . Shughuli hizo ni pamoja na utoaji wa nyongeza ya matone ya Vitamin A, dawa za minyoo na upimaji wa lishe kwa watoto chini ya miaka 5 uliofanyika katika kampeni ya mwezi Disemba 2023 kwa watoto 67,959 kati ya watoto waliotegemewa 67,951 sawa na 100.01%.
Shughuli zingine ni utoaji wa vidonge vya kuongeza wingi wa damu (FEFO) kwa wajawazito wanahudhuria kliniki katika vituo vya kutolea huduma za afya, upimaji wa hali ya lishe na matibabu ya utapiamlo mkali, utoaji wa elimu ya unyonyeshaji na unasihi wa ulishaji sahihi wa chakula cha nyongeza kwa watoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha kuwa wanasimamia uanzishaji vitalu vya viazi lishe katika maeneo ya shule na kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe ya Wilaya ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo ili kuwezesha mafanikio katika mpango wa Taifa wa masuala ya Lishe.
Mpango wa upatikanaji wa chakula mashuleni ni mojawapo ya afua inayolenga kuongeza afya za wanafunzi na kupunguza utoro mashuleni ikiwa ni Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe “National Multasectoral Nutrition Action Plan” (NMNAP) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Lishe na Mkakati wa miaka kumi (2015/16 – 2025/26). Mpango huo umeainisha afua mbalimbali za lishe zinazopaswa kutekelezwa nchini kwa lengo la kupambana na utapiamlo katika aina zake zote.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Johari Samizi akifungu kikao cha Tathmini
ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Disemba, 2023
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Shinyanga Machi 01, 2024
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Lishe wakifuatilia kwa makini wakati wa kikao hicho
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Bw. Said Mankligo akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Disemba, 2023
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.