Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mh. Isack Sengerema leo tarehe 03/02/2022 ameongoza shughuli ya utoaji wa Hundi ya Mfano kwa Vikundi vya Wanawake, Vjana na Watu wenye Ulemavu yenye thamani ya Kiasi cha Shs. 173,808,661 (Millioni mia moja sabini na tatu, mia nane na nane elfu na mia sita sitini na moja) kwa Vikundi hivo.
Akiongea kwenye Hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Nice R. Munissy, alisisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuona wananchi wanapiga hatuwa kiuchumi hivo alimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa Maelekezo yake juu ya kutowa Asilimia 10 ya Mapato ya Ndani kwa vikundi vya kina Mama, Vijana na Watu wenye Ulemavu katika Halmashauri, alianza hotuba yake kwa Kuwashukuru wadau wa Maendeleo waliohudhuria Hafla hiyo, Benki ya CRDB, Mh Awadh, Diwani wa Kata ya Solwa na Mgeni Rasmi Mh ISack Sengerema, Diwani wa Iselamagaza na Makamu Mwenyekiti. alieleza kuwa Mwaka huu walipanga kutowa kiasi cha Shs Milioni 192 lakini juhudi za Ukusanyaji Mapato zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga zimepelekea mpaka sasa kuweza kutowa Kiasi cha Shs 173, 808, 661 kwa Vikundi hivo.
Alieleza kuwa ni lazima Kina Mama, Vijana na Watu wenye Ulemavu wajitokeze kukopa fedha hizi kwani hazina riba unachukuwa kiasi ndio hiko hiko utakirudisha. mheshimiwa Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Halmashauri inatamani kuona watu wengi zaidi wanapata hela zaidi kwani Halmashauri inakusudia kuongeza Mapato yake maradufu ili hizi pesa wanazozitowa nazo ziweze kuzidi maradufu na makundi hayo yalisistizwa kuchangamkia Fursa.
Alisisitiza kuwa nia ya Serikali na ya Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi tunakwamuka na kuwa Uchumi wa Kati uendane na kukwamuka kwa pato la kila mwananchi hapa Nchini. akasisitiza kuwa ndio maana leo wameona watowe kiasi hiko cha Shs. Milion 173 na Laki 6 kwa Vikundi ili viweze kujikwamuwa Kiuchumi.
MKurugenzi huyo Aliwaomba Walemavu wajitokeze kuja kukopa pesa hizo kwani inaonekana muamko wao kuja kukopa ni mdogo japo alisema wapo wachache walemavu walikuja kukopa na kuwa wanaendelea vizuri na biashara za walizozianzisha. " Tunawataka nyie mnaochukuwa fedha hizi leo, mkawe Mabalozi wazuri kwa wengine, mfanye kazi na faida za kuonekana na kurejesha fedha kwa wakati ili wengine waweze waiga" Alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Halmashauri.
Alimalizia kwa kusema kuwa hizi pesa zinatolewa kwa sababu kumekuwa na juhudi kubwa katika Ukusanyaji wa Mapato na kuwaomba wana Vikundi hao kuwa wasikubali kuona mtu anapoteza mapato au ushuru wa Halmashauri na kumuacha salama kwani ni kutokana na tozo hizi ndio Halmashauri inaweza kusanya hizi fedha na kuwapatia wao wafanye Miradi yenye Tija. alimalizia kwa kumakaribisha Mheshimiwa Mgeni Rasmi aweze kuongea na Hadhara.
Akiongea Makamu Mwenyekiti alisema anampongeza sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Juhudi zake za kuongeza Mapato na kuwa sasa wameweza hadi kuvunja Rekodi ya utoaji fedha hizi za mikopo isiyo na Riba kwa makundi hayo.
Aliwataka Wananchi hawa wafaidika wa Mikopo kusaidia Halmashauri kwenye kukusanya tozo mbali mbali kwani ni pesa hizo zilizokusanywa ndio zimewezesha wao kupatiwa mitaji hiyo ambayo alisisitiza wakiitumia vizuri kufanya kazi kwa Malengo basi wanatoka kimaisha.
Alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kuwakusanya wanufaika wote wa Mikopo hii, ili wakutane na wataalam wa Masoko wa CRDB Bank na Wananchi wachache wanufaika wa Mikopo hii waliofanikiwa ili waweze kukutanishwa na kupeana uzoefu kwenye kuendesha Miradi hii itokanayo na fedha za mikopo. " Mheshimiwa Mkurugenzi nkuombe siku moja, uandae Chakula na kuwaita watu wa makundi yote na wataalam wa CRDB na wanufaika ili waweze kubadilishana Uzoefu na kuwapa Mbinu ambazo wengine wamefanikiwa na kuwa wafanya baishara wakubwa.
Alimalizia kwa kumpongeza sana Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa Usimamizi Mzuri wa hizi pesa na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni watu wale hawajajikomboa kiuchumi. " Kiukweli nimshukuru na Kumpongeza sana Ndg Deus Mhoja, hizi Fedha zamani zilikuwa zinaliwa na watu Wajanja wajanja tu lakini sasa hivi zimewafikia hadi watu wa Ngumango huko ndani nawaona hapa" Alisisitiza Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
Vijana, Kina Mama na Wanufaika wote wa Mikopo hiyo walimalizia kwa kuwashukuru sana Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na kuahidi kuwa watafanya marejesho kwa wakati na kuhakikisha hizo pesa zinarudi ili zije kuwanufaisha wengine kama wao walivonufaika.
NIndo - Iselamagazi
Anuani ya posta: 113 Shinyanga
Simu: 0282-986382
Simu: 0282-986382
Baruapepe za watumishi: info@shinyangadc.go.tz/ded@shinyangadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.